90. Sunnah ni kuzika makaburini na uharamu kuzikana nyumbani

89- Sunnah ni kuzika makaburini. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwazika wafu kwenye makaburi ya al-Baqiy´. Kama ambavo kumepokelewa khabari nyingi juu ya hilo. Kumekwishatangulia baadhi yake katika minasaba mbalimbali. Mnasaba wa karibu zaidi ni Hadiyth ya Ibn-ul-Khaswaaswiyah ambayo nimeitaja katika masuala yaliyopita. Hainukunuliwa kutoka katika yeyote kutoka kwa Salaf kwamba alizikwa kusipokuwa makaburini. Iispokuwa yale yaliyopokelewa kwa njia nyingi vilevile kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alizikwa chumbani mwake. Hilo ni miongoni mwa mambo ambayo ni maalum kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hayo yamefahamishwa na Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) aliyeeeleza:

“Wakati ilipochukuliwa roho ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walitofautiana juu ya kumzika. Abu Bakr akasema: “Nimesikia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) jambo ambalo sijalisahau. Amesema: “Allaah hatochukua roho ya Nabii yeyote isipokuwa mahala ambapo anapenda azikwe mahala hapo.” Hivyo wakamzika mahala palipokuwa godoro lake.”

 Ameipokea at-Tirmidhiy (02/129) ambaye amesema:

“Hadiyth ni geni. ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Bakr al-Mulaykiy ni mwenye kudhoofishwa upande wa kumbukumbu yake.”

Lakini Hadiyth imethibiti kutoka katika njia mbalimbali na shawahidi:

1- Ameipokea Ibn Maajah (01/489, 499), Ibn Sa´d (02/71) na Ibn ´Adiyy katika “al-Kaamil” (Makhtuta 02/94) kupitia kwa Ibn ´Abbaas kutoka kwa Abu Bakr.

2- Ibn Sa´d na Ahmad (nambari. 27) kupitia njia mbili zilizokatika kutoka kwa Abu Bakr.

3- Ameipokea Maalik (01/230) na Ibn Sa´d kutoka kwake kwa njia ya kufikiwa na khabari.

4- Ameipokea Ibn Sa´d kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kutoka kwa Abu Bakr kwa ufupi na kutoka kwa Swahabah. Lakini hata hivyo ina hukumu ya kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kadhalika ameipokea at-Tirmidhiy katika  “ash-Shamaa-il” (02/272) katika kisa cha kufa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

al-Haafidhw Ibn Hajar amesema (01/420):

“Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh. Lakini hata hivyo ni yenye kuishilia kwa Swahabah. Ambayo iko kabla yake iko wazi zaidi katika malengo. Pindi tendo litafasiriwa kwamba ni jambo maalum, basi haitokuwa mbali kukatazwa mwengine kutokamana na jambo hilo. Bali ndio jambo lenye mwelekeo. Kwa sababu kuendeleza jambo la kuzika majumbani pengine likayageuza majumba kuwa makaburi. Hivyo kuswali ndani yake itakuwa ni jambo lililochukizwa.”

al-Bukhaariy amenyofoa hukumu ya machukizo kutoka katika maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Jaalieni baadhi swalah zenu kuziswali majumbani mwenu na wala msiyafanye ni makaburi.”

Ameitaja katika “Mlango unaozungumzia machukizo ya kuswali makaburini.”

kutoka katika Hadiyth ya Ibn ´Umar. al-Haafidhw akasema:

“Tamko la Hadiyth ya Abu Hurayrah kwa Muslim liko wazi zaidi kuliko HAdiyth iliyotajwa katika mlango. Nalo ni maneno yake:

“Msiyafanye majumbani yenu kuwa ni makaburi.”

Kwani hakika udhahiri wake unapelekea makatazo ya kuzikana majumbani moja kwa moja.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 173-175
  • Imechapishwa: 16/02/2022