Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:

“Sunnah hailinganishwi na kitu kingine.”

Unapojiwa na dalili jisalimishe:

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Naapa kwa Mola wako! Hawatoamini mpaka wakufanye wewe kuwa mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao kisha wasipate katika nyoyo zao kipingamizi katika yale uliyohukumu na wajisalimishe ukweli wa kujisalimisha.”[1]

Pindi mtu anapokutajia dalili iliyothibiti na sahihi basi hutakiwi kuleta hoja hizi na zile na kufanya malinganisho. Abu Hurayrah amepokea Hadiyth:

“Mwenye kula kitu chenye kupikwa anatakiwa kutawadha.”

Ndipo mtu mmoja akamuuliza: “Je, nitawadhe kwa maji ya moto?” Abu Hurayrah akamjibu kwa kumwambia: “Ee mwana wa ndugu yangu! Ninapokueleza Hadiyth kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi usiilinganishe na kitu.”[2]

[1] 04:65

[2] Ibn Maajah (22).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 371-372
  • Imechapishwa: 23/07/2017