Faida ya nne: Wakati Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walipomuuliza Mutme wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni namna gani wanavyotakiwa kumsifu akawafunza ile du´aa ya kwanza. Ni dalili inayofahamisha kuwa ndio kumsifu kuliko bora (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sababu hajichagulii juu ya nafsi yake isipokuwa kilicho kitukufu na bora zaidi. Kutokana na hayo an-Nawawiy amesema katika “Rawdhwat-ut-Twaalibiyn” kwamba lau mtu ataapa kwa Allaah kwamba atamsifu yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa njia iliyo bora kabisa, basi atakuwa hakutimiza kiapo chake kama hakumsifu kwa njia zilizotajwa hapo juu. as-Subkiy amesema kwamba yule mwenye kumsifu kwa njia hizo basi atakuwa amehakikisha kweli kuwa amemsifu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilihali sifa zengine zote ni zenye kutia wasiwasi. Wakati Maswahabah walipomuuliza ni vipi wamsifu akasema: “Semeni:

اللهم صل على محمد و على آل محمد كما صليت على إبراهيم [و آل إبراهيم]، إنك حميد مجيد. و بارك على محمد و على آل محمد كما باركت على [إبراهيم و]آل إبراهيم، إنك حميد مجيد

“Ee Allaah! Msifu Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyomsifu Ibraahiym [na jamaa zake Ibraahiym]. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa. Ee Allaah! Na mbariki Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki [Ibraahiym] na jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”

Kwa hiyo hivi ndivo wanavyotakiwa kumswalia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). al-Haythamiy ameyataja haya katika “ad-Durr al-Mandhuud”[1]. Halafu akataja kwamba lengo litakuwa limefikiwa kwa njia zote zilizotajwa katika Hadiyth Swahiyh[2].

[1] 02/25.

[2] 01/27.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 152-153
  • Imechapishwa: 07/01/2019