88. Hadiyth ”Siku moja al-Waliyd bin ´Uqabah… ”

88 – Muslim bin Ibraahiym ametuhadithia: Hishaam bin Abiy ´Abdillaah ad-Dastawaa-iy ametuhadithia: Hammaad bin Abiy Salmaan ametuhadithia, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Alqamah, ambaye ameeleza:

”Siku moja al-Waliyd bin ´Uqabah alimwendea Ibn Mas´uud, Abu Muusa na Hudhayfah kabla ya ´iyd na akawaambia: ”´Iyd hii imekaribia. Ni vipi kuleta Takbiyr ndani yake?” ´Abdullaah akasema: ”Unaanza kwa kuleta Takbiyr unayofungua kwayo swalah, unamuhimidi Mola wako na unamswalia Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kisha unaomba du´aa au kuleta Takbiyr na ufanye vivyo hivyo. Kisha utaleta Takbiyr na ufanye vivyo hivyo. Halafu usome. Kisha utaleta Takbiyr na kwenda katika Rukuu´. Kisha utasimama, utasoma na kumhimidi Mola wako na umswalie Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kisha utaomba du´aa, kumkabiri Allaah na ufanye vivyo hivyo. Kisha utaleta Takbiyr na ufanye vivyo hivyo. Halafu utarukuu.” Hudhayfah na Abu Muusa wakasema: ”Amesema kweli Abu ´Abdir-Rahmaan.”[1]

89 – ´Aliy bin al-Madiyniy ametuhadithia Hadiyth hiihii, kutoka kwa Khâlid bin al-Haarith, kutoka kwa Hishaam, ambapo humo amesema:

”Kisha utaleta Takbiyr na kwenda katika Rukuu´.” Hudhayfah na al-Ash´ariy wakasema: ”Amesema kweli Abu ´Abdir-Rahmaan.”[2]

[1] Cheni ya wapokezi ni nzuri. Wapokezi wote ni wapokezi wa al-Bukhaariy na Muslim – isipokuwa tu Hammaad bin Abiy Sulaymaan, ambaye ni mpokezi wa Muslim peke yake. Haafidhw amesema juu yake katika ”at-Taqriyb”:

”Ni mwenye kuaminika na anakosea.”

as-Sakhaawiy katika “al-Qawl al-Badiy´” amesahihisha cheni ya wapokezi wake.

[2] Cheni ya wapokezi ni nzuri kama ile ilio kabla yake.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 77-78
  • Imechapishwa: 12/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy