89. Athar ”Tulikuwa Khayf pamoja na… ”

90 – Sulaymaan bin Harb ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdullaah bin Abiy Bakr, ambaye ameeleza:

”Tulikuwa Khayf[1] pamoja na ´Abdullaah bin Abiy ´Utbah. Akamuhimidi Allaah na kumsifu, akamswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akaomba du´aa. Kisha baadaye akasimama na kutuswalisha.”[2]

[1] Ni maeneo Minaa karibu na nguzo za kutupa vijiwe.

[2] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. ´Abdullaah bin Abiy ´Utbah al-Answaariy al-Baswriy alikuwa ni mtumwa wa Anas aliyemwacha huru. ´Abdullaah bin Abiy Bakr ni Ibn Muhammad bin ´Amr bin Hazm al-Answaariy al-Qaadhwiy. Wote wawili ni miongoni mwa ambao al-Bukhaariy anawatumia kama hoja.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 78
  • Imechapishwa: 12/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy