87. Athar ”´Umar alikuwa akileta Takbiyr tatu katika Swafaa na akisema… ”

87 – Hudbah bin Khaalid ametuhadithia: Hammaam bin Yahyaa ametuhadithia: Naafiy´ ametuhadithia:

”´Umar alikuwa akileta Takbiyr tatu katika Swafaa na akisema:

لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, ufalme ni Wake, himdi zote njema ni Zake, Naye juu ya kila jambo ni muweza.”

Kisha anamswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akiomba du´aa na akirufusha kisimamo na du´aa halafu baadaye anafanya vivyo hivyo Marwah.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi imekatika, kwa sababu Naafiy´ hakuwahi kukutana na ´Umar. Hata hivyo mtunzi amenukuliwa katika ”Jalaal-ul-Afhaam” kumtaja Ibn ´Umar. Ikiwa haya yamesihi, basi neno ”Ibn” limetoweka katika nuskha yetu. Katika hali hiyo cheni ya wapokezi itakuwa yenye kuungana na Swahiyh, lakini ninapata uzito wa kuona hivo – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 76-77
  • Imechapishwa: 12/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy