86. Athar “Niseme nini nikiingia msikitini?”

86 – ´Aarim bin al-Fadhwl ametuhadithia: Hammaad bin Zayd ametuhadithia, kutoka kwa Mansuur al-Mu´tamir, kutoka kwa Yaziyd bin Dhiy Huddaan, ambaye amesema:

”Nilimwambia ´Alqamah: ”Ee Abu Shibl! Niseme nini nikiingia msikitini?” Sema: ”Allaah na Malaika wake wamsifu Muhammad! Amani iwe nawe, ee Mtume, na rehema za Allaah.” Nikasema: ”Ni nani aliyekuhadithi? Wewe ndiye uliyasikia?” Akasema: ”Hapana. Amenihadithia nayo Abu Ishaaq al-Hamadaaniy.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni dhaifu. Sijapata aliyemtaja Yaziyd bin Dhiy Huddaan. Pengine ni ndugu yake na Sa´iyd bin Dhiy Huddaan katika cheni ya kabla yake au ni kosa la uchapishaji kati ya Sa´iyd na Yaziyd – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 76
  • Imechapishwa: 12/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy