85. Athar ”Niseme nini ninapoingia msikitini?”

85 – Sulaymaan bin Harb ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq: Nimemsikia Sa´iyd bin Dhiy Huddaan akisema:

”Nilimwambia ´Alqamah: ”Niseme nini ninapoingia msikitini?” Akasema: ”Sema: ”Allaah na Malaika wake wamsifu Muhammad! Amani iwe nawe, ee Mtume, rehema za Allaah na baraka Zake.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni dhaifu. Sa´iyd bin Dhiy Huddaan hatambuliki. Katika ”Jalaa’-ul-Afhaam”, uk. 81, imekuja Sa´iyd bin Jarraan, nalo ni kosa la uchapishaji.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 75-76
  • Imechapishwa: 12/02/2024