Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Hali kadhalika kuhusu yale tuliyoyataja kuhusu kupigwa vita mayahudi na Maswahabah kuwapiga vita Banuu Haniyfah. Hali kadhalika alitaka Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwavamia Banuu al-Mustwalaq baada ya kuambiwa na mtu kutoka katika wao ya kwamba wamekataa kutoa zakaah. Mpaka Allaah kateremsha:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا

“Enyi mlioamini! Anapokujieni fasiki kwa habari yoyote, basi kwanza pelelezeni.” (49:06)

Ikaonekana ya kwamba mtu huyo amewasemea uongo[1]. Yote haya yanaonesha dalili ya kwamba makusudio ya Mtume (Swalla Allaah ´alayhi wa sallam) kwa Hadiyth ambazo wanatumia kama hoja, [ni haya] tuliyoyataja.

MAELEZO

Bi maana kutamka Shahaadah ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah sio kizuizi kabisa cha kutouawa. Uhakika wa mambo ni kwamba inajuzu kumpiga vita mwenye kusema hivo ikiwa kuna sababu zenye kupelekea katika hilo.

[1] Imepokelewa na at-Twabariy (27/123) na Ibn Kathiyr (04/187) na kusema:

“Hadiyth hii imepokelewa kwa njia nyingi. Miongoni kwa ilio bora zaidi ni ile iliyopokelewa na Ahmad.”

al-Haythamiy amesema:

“Imepokelewa na Ahmad na wanaume wake ni waaminifu.” (Majmuu´-uz-Zawaaid (07/111))

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 95-96
  • Imechapishwa: 28/11/2023