Kuhusu kafiri hautofaa kitu uombezi:

مَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ

“Madhalimu hawatokuwa na rafiki na wala mwombezi anayetiiwa.”[1]

فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ

“Basi haitowafaa uombezi wowote wa waombezi.”[2]

Ndani ya Qur-aan kuna sampuli mbili za uombezi: uombezi uliokanushwa na uombezi uliothibitishwa. Uombezi uliokanushwa ni ule ambao haukukamilisha sharti zake na uombezi uliothibitishwa ni ule ambao umekamilisha sharti zake. Kafiri hautomfaa kitu uombezi hata kama ataombewa na wakazi wote wa mbinguni na wa ardhini, basi Allaah hatowakubalia uombezi wao. Kwa sababu ni mshirikina ambaye amemkufuru Allaah (´Azza wa Jall). Allaah hakubali maneno wala matendo yake. Isipokuwa tu ule uombezi ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atamwombea ami yake Abu Twaalib. Huu ni uombezi maalum. Isitoshe hatoombewa ili atoke Motoni, ni uombezi ili mtu huyu apunguziwe adhabu kutokana na vile alivyomnusuru, kumhami na kumtetea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atamwombea ili apunguziwe adhabu peke yake.

[1] 40:18

[2] 74:48

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 97-98
  • Imechapishwa: 25/01/2023