al-Qummiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يُزَكُّونَ أَنفُسَهُم ۚ بَلِ اللَّـهُ يُزَكِّي مَن يَشَاءُ وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًا

“Je, hukuwaona wale wanaojitakasa nafsi zao?  Bali Allaah anamtakasa amtakaye na wala hawatodhulumiwa kiasi cha kijiuzi kilichomo ndani ya uwazi wa kokwa ya tende.”[1]

“Maneno Yake:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يُزَكُّونَ أَنفُسَهُم

“Je, hukuwaona wale wanaojitakasa nafsi zao?”

inawalenga wale wenye kujiita “as-Swiddiyq”, “al-Faaruq” na “Dhun-Nuurayn”.”[2]

Aayah inawahusu mayahudi na manaswara waliosema kuwa wao ndio wana na wapenzi wa Allaah.

وَقَالُوا لَن يَدْخُلَ الْجَنَّةَ إِلَّا مَن كَانَ هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ

“Walisema: “Hatoingia Peponi isipokuwa aliyekuwa myahudi au mnaswara.”[3]

وَقَالُوا لَن تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَّعْدُودَةً

“Walisema: “Hautatugusa Moto isipokuwa siku chache tu.”[4]

Raafidhwah wamefanana nao pindi wanapojitakasa wenyewe na kumzulia Allaah uongo, ´Aliy na familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ngazi yao ya uongo inashinda uongo wa mayahudi na manaswara.

Ama kuhusu as-Swiddiyq, al-Faaruq na Dhun-Nurayn (Radhiya Allaahu ´anhum) hawakujitakasa wao wenyewe kwa majina haya; Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye na waumini wakweli ndio waliofanya hivo.

al-Qummiy amesema:

“Maneno Yake:

وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًا

“… na wala hawatodhulumiwa kiasi cha kijiuzi kilichomo ndani ya uwazi wa kokwa ya tende.”[5]

Bi maana kijiuzi kilichomo ndani ya kokwa ya tende. Halafu akawazungumzia kwa njia ya kuashiria na kusema: “Tazama namna wanavyomzulia Allaah uongo ilihali wamewapokonya familia ya Muhammad haki yao.”[6]

1- as-Swiddiyq, al-Faaruq na ´Uthmaan Dhun-Nurayn (Radhiya Allaahu ´anhum) hawakujitakasa wao wenyewe. Walikuwa ni miongoni mwa watu wanaomcha Allaah zaidi. Mwenye kusema historia anatambua hilo. Abu Bakr hakusema:

“Mimi ni as-Swiddiyq (mkweli sana).”

´Umar hakusema:

“Mimi ni al-Faaruuq (anayepambanua kati ya haki na batili).”

´Uthmaan hasema:

“Mimi ni Dhun-Nurayn (aliye na nuru mbili).”

Waliosema hivo ni waumini waliozitambua hali zao, nafasi zao, tabia zao na matendo yao. Hiyo ni bishara ya muumini ya mapema, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[7]. Maswahabah wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walishuhudia kuwa watatu hawa ndio wabora wa Ummah. Kumepokelewa mapokezi tele kutoka kwa ´Aliy ya kwamba Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ni bora kuliko yeye.

2- Makhaliyfah watatu hawakuipokonya familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) chochote katika haki zao. Bali walikuwa wakiwakirimu. ´Umar alikuwa akilitanguliza kabila la Haashim kabla ya kabila lake, Banu ´Adiyy, na akimtanguliza mbele mtumwa wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Usaamah kabla ya mwanae ´Abdullaah.

3- Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio watu bora wa Ummah. Wao ndio walikuwa wachaji Allaah na wakweli sana. Haikujilikana kwa wao kusema uongo. Ni vipi Baatwiniyyah wanaweza kusema kuwa wanamzulia Allaah uongo? Hakika watu hawamjui mwongo mkubwa kama Raafidhwah na khaswa khaswa Baatwiniyyah wao huyu mwongo na mtenda dhambi.

[1] 04:49

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/140).

[3] 02:111

[4] 02:80

[5] 04:49

[6] Tafsiyr al-Qummiy (1/140).

[7] Bali Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Juu yako yuko Mtume, mkweli sana na shahidi.”

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intisaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 130-131
  • Imechapishwa: 20/11/2017