86. Ni nani ambaye ana haki ya umoja, kusikilizwa na kutiiwa?

Swali 86: Ni nani ambaye ana haki ya umoja, kusikilizwa na kutiiwa?

Jibu: Ambaye anayo haki ya kusikilizwa na kutiiwa kwa waislamu wote ni watawala katika viongozi na wanazuoni, muda wa kuwa ni katika mema. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ

“Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.”[1]

Wakati mtawala wa waislamu anapotiiwa kunapatikana umoja na kunaondoka migawanyiko. Kuhusu wambea na wanafiki haifai kuwatii[2]. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ اتَّقِ اللَّـهَ وَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَالْمُنَافِقِينَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا

”Ee Nabii! Mche Allaah na wala usiwatii makafiri na wanafiki. Hakika Allaah daima ni Mjuzi wa kila jambo, Mwenye hekima!”[3]

وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ هَمَّازٍ مَّشَّاءٍ بِنَمِيمٍ مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ

”Na wala usimtii kila mwingi wa kuapa, mtwevu, mwingi wa kukashifu, mpitaji huku na huku akieneza uvumi, mwingi wa kuzuia ya kheri, mwenye kuvuka mipaka, mwingi wa kutenda dhambi… ”[4]

[1] 4:59

[2] Utiifu huu unafanana na ule unaofanyika leo hii kati ya vyama na mapote ya kisiasa na wafuasi wake. Wafuasi wanakula viapo vya utiifu kwa wale viongozi wa mapote na vyama ambapo hawatoki nje ya amri zao na sambamba na hilo wanaacha kumtii mtawala. Wako watu ambao wanaeneza viapo vya mapote haya ya Hizbiyyah na ya kizushi. Mwenye kanda ”al-Islaam wal-Hizbiyyah” amesema:

”Kuhusu viapo utifuu wanavyopewa makundi ya kiislamu, naona kuwa angalau kwa uchache kuwa vinachukiza kwa sababu vinafanana na nadhiri. Hiyo ni ijtihaad yangu mwenyewe na simlazimsihi yeyote kuona hivo.”

[3] 33:1

[4] 68:10-12

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 213-214
  • Imechapishwa: 29/07/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy