Swali 87: Je, umoja unafikiwa kwa kuleta uchochezi na kuweka chuki ndani ya mioyo ya watu wa kawaida dhidi ya watawala?
Jibu: Mambo hayo yanafanywa na waharibifu na wambea ambao wanataka kueneza vurugu na machafuko kwenye jamii ya Kiislamu. Hapo zamani wanafiki walijaribu kufanya kitu kama hicho pale ambapo kuwatenganisha waislamu kutokana na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili jamii isambaratike[1]. Walisema:
لَا تُنفِقُوا عَلَىٰ مَنْ عِندَ رَسُولِ اللَّـهِ حَتَّىٰ يَنفَضُّوا
”Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Mtume wa Allaah mpaka watokomee mbali.”[2]
Kujaribu kutenganisha kati ya watawala na wananchi ni miongoni mwa matendo ya wanafiki ambao wanaeneza ufisadi ardhinini. Allaah (Ta´ala) amesema juu yao:
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ
”Na wanapoambiwa ´Msifanye ufisadi katika ardhi`, basi husema ´Hakika sisi ni watengenezaji`.”[3]
Yule ambaye anawataki mema watawala na wananchi wanakuwa kinyume na hivo. Hufanya bidii ili wananchi wawapende watawala wao na watawala wawapende wananchi, kuleta umoja na kujiepusha na kila kinachopelekea katika tofauti.
[1] Wao ndio kufanya uchochezi dhidi ya watawala ilihali wao wenyewe hawafanyi uasi. Wanazuoni wamewaita kuwa ni wakaaji (القعدية). Wakati Ibn Hajar (Rahimahu Allaah) alipokuwa akiyataja mapote potevu akawataja wakaaji na akasema:
”Wale wanaopambia kuwafanyia uasi watawala wala wao hawafanyi.” (Fath-ul-Baariy (1/459))
Vilevile amesema:
”Hawakuwa wakitambulika kupambana bali wanawakemea watawala wenye kudhulumu kwa kiasi cha uwezo, wakilingania katika fikira yao na wakipambia jambo la kufanya uasi.” (Tahdhiyb-ut-Tahdhiyb (8/114))
Wakaaji ni kipote miongoni mwa Khawaarij kama tulivosema. Kwa ajili hiyo asifikirie mwenye kufikiria kuwa Khawaarij pekee ni wale wanaofanya uasi kwa upanga dhidi ya mtawala. Ibn Hajar (Rahimahu Allaah) amesema wakati alipokuwa akiwataja watu ambao katika ´Aqiydah zao:
”´Imraan bin Hittwaan. Alituhumiwa kuwa katika wakaaji katika Khawaarij.” (Fath-ul-Baariy (1/460))
Mara nyingi wakaaji wanakuwa khatari zaidi kuliko Khawaarij. Kwa sababu uchochezi dhidi ya watawala unakuwa na athari kubwa zaidi, khaswa pale ambapo jambo hilo linafanywa na mtu mwenye ufaswaha na mwenye kujidhihiirisha Sunnah. ´Abdullaah bin Muhammad adh-Dhwa´iyf (Rahimahu Allaah) amesema:
”Khawaarij wakaaji ndio Khawaarij wabaya zaidi.” (Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 271, ya Abu Daawuud)
[2] 63:07
[3] 2:11
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 214-216
- Imechapishwa: 29/07/2024
- taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 214-216
Imechapishwa: 29/07/2024
taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
https://firqatunnajia.com/87-je-umoja-unafikiwa-kwa-kufanya-uchochezi-dhidi-ya-watawala/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)