86. Anayefanya I´tikaaf kuepuka maongezi ya kilimwengu

Malengo ya I´tikaaf ni mtu kujitenga na watu kwa ajili ya kupata muda wa kumtii Allaah msikitini miongoni mwa misikiti yake kwa ajili ya kutafuta thawabu zake na pia kutafuta usiku wa makadirio. Kwa ajili hiyo mwenye kufanya I´tikaaf anapaswa kujishughulisha kufanya Dhikr, kusoma Qur-aan, kuswali na ´ibaadah nyenginezo. Aidha anatakiwa kujiepusha na mambo yasiyomuhusu katika maongezi ya kilimwengu. Hapana vibaya akaongea kidogo maongezi yanayofaa pamoja na familia yake au wengineo kutokana na manufaa. Swafiyyah, mama wa waumini, (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa amekaa I´tikaaf. Nikamjilia kumtembelea usiku. Nikamzungumzisha. Kisha nikasimama ili niondoke (kurudi nyumbani). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasimama pamoja nami… ”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 157
  • Imechapishwa: 11/03/2024