82. Waumini wote wako Peponi na makafiri wote wako Motoni

Vivyo hivyo lau mtu atakuwa kafiri au mtenda madhambi hatumshuhudilii Moto. Kwa sababu hatujui atamalizia vipi. Hatumshuhudilii yeyote Pepo hata kama ni miongoni mwa waja wema. Kwa sababu hatujui mwisho wake atamalizia vipi. Na wala hatumshuhudilii yeyote Moto hata kama ni kafiri. Kwa sababu hatujui mwisho wake atamalizia vipi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mja atafanya matendo ya watu wa Motoni mpaka kusiwe kati yake yeye na hiyo isipokuwa dhiraa akatanguliwa na kitabu ambapo akafanya matendo ya watu wa Peponi n aakaingia ndani yake. Hakika mtu atafanya matendo ya watu wa Peponi mpaka kusiwe kati yake yeye na hiyo isipokuwa dhiraa akatanguliwa na kitabu ambapo akafanya matendo ya watu wa Motoni aakaingia ndani yake.”[1]

Mtu atavyomalizia hakuna anayelijua isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Sisi hatumshuhudilii mtu kwa dhati yake. Ama ujumla sisi tunashuhudia juu ya makafiri kwamba wako Motoni bila ya kumlenga fulani. Tunasema kuwa makafiri wako Motoni na waumini wako Peponi kwa ujumla. Amesema (Ta´ala) kuhusu Pepo:

أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ

“Imeandaliwa kwa wenye kumcha Allaah.”[2]

Amesema kuhusu Moto:

أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ

”Umeandaliwa kwa makafiri.”[3]

Hapana shaka kwamba makafiri wako Motoni pasi na kumlenga mtu isipokuwa kwa ushahidi. Hapana shaka kwamba waumini wako Peponi bila ya kuwalenga watu kwa dhati yake isipokuwa kwa ushahidi kutoka kwa yule ambaye hazungumzi kwa matamanio. Huku ni kufanya adabu pamoja na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Sisi hatumshuhudilii yeyote isipokuwa kwa dalili. Lakini tunatarajia kwa mtenda mema na tunachelea juu ya mtenda maovu.

[1] al-Bukhaariy (3208) na Muslim (2643) kupitia kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh).

[2] 03:133

[3] 03:131

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 116
  • Imechapishwa: 25/05/2021