Hakuna wataovuka Njia isipokuwa waumini kwa kiasi cha matendo yao. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya Abu Sa´iyd (Radhiya Allaahu ´anh) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na humo imekuja:

“Waumini watapita kama kupepesa kwa macho, kama umeme, kama upepo, kama ndege, kama farasi wa kasi na bora. Kuna watakaookoka na kusalimishwa, wengine watakwaruzwa kisha waachiliwe na kuna wataotupwa Motoni.”

Kuna maafikiano juu yake.

Imekuja katika “as-Swahiyh” ya Muslim:

“Matendo yao ndio yatawavukisha na Mtume wenu amesimama juu ya Njia huku akisema: “Ee Mola wangu! Salimisha! Salimisha” mpaka yatashindwa matendo ya waja kiasi cha kwamba atakuja mtu na asiweze kuvuka isipokuwa kwa kutambaa.”[1]

Imekuja katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy:

“Mpaka atapita wa mwisho wao ambapo atavutwa kwelikweli.”[2]

Wa kwanza atakayevuka Njia katika Mitume ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na miongoni mwa nyumati ni Ummah wake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nitakuwa mimi na Ummah wangu ndio wa kwanza watakaoivuka na siku hiyo hakuna wataozungumza isipokuwa Mitume na du´aa ya Mitume siku hiyo ni: “Ee Allaah! Salimisha! Salimisha!”[3]

Ameipokea al-Bukhaariy.

[1] Muslim (195, 329).

[2] al-Bukhaariy (7439). 

[3] al-Bukhaariy (7437).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 127-128
  • Imechapishwa: 04/12/2022