Aliulizwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu njia ambapo akasema:

“Ni yenye kutelezesha na juu yake kuna makucha ya wanyama wakali, makucha kama ya mbwa na miba ilio sawa na mipana na ina miba inayoweza kuua mbuzi inakuweko Najd inaitwa “as-Sa´daan.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy.

Amepokea tena kutoka katika Hadiyth ya Abu Hurayrah:

“… ina makucha kama ya mbwa mfano wa makucha ya mti huyo wa as-Sa´daan licha ya kwamba hakuna anayejua ukubwa wake isipokuwa Allaah. Itawapora watu kutegemea matendo yao.”[2]

Katika “as-Swahiyh” ya Muslim kutoka katika Hadiyth ya Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesema:

“Nimefikiwa na khabari ya kwamba [hiyo Njia] ni nyembamba sana kuliko nywele na ina makali sana kuliko upanga.”[3]

Imaam Ahmad amepokea mfano wake kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] Ni sehemu ya Hadiyth ya Abu Sa´iyd al-Khudriy iliyokwishatangulia aliyoipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[2] al-Bukhaariy (6573) na Muslim (182, 299).

[3] Muslim (183, 302) iliyokwishatangulia.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 126-127
  • Imechapishwa: 04/12/2022