Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Njia ni haki. Wema watavuka na waasi watatumbukia humo.

MAELEZO

Njia maana yake kilugha ni njia hivohivo. Njia maana yake katika Shari´ah ni daraja itayowekwa juu ya Moto ili watu wapite juu yake kuelekea Peponi. Ni kitu kimethibiti kwa Qur-aan, Sunnah na maneno ya Salaf. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا

“Na hakuna yeyote miongoni mwenu isipokuwa ataufikia.”[1]

´Abdullaah bin Mas´uud, Qataadah na Zayd bin Aslam wamefasiri kuwa ni kupita juu ya Njia. Kuna kikosi katika wao, akiwemo Ibn ´Abbaas, ambao wamefasiri kwamba ni kuingia ndani ya Moto lakini baadaye wataokolewa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kisha itawekwa daraja juu ya Moto na utashuka uombezi na watasema: “Ee Allaah! Tusalimishe! Tusalimishe!”[2]

Kuna maafikiano juu yake.

Ahl-us-Sunnah wameafikiana juu ya kuthibiti kwake.

[1] 19:71

[2] al-Bukhaariy (7439) na Muslim (183, 302).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 125-126
  • Imechapishwa: 04/12/2022