80. Athar ”Mbapopita katika misikiti… ”

80 – Yahyaa bin ´Abdil-Hamiyd ametuhadithia: Sayf bin ´Umar at-Tamiymiy ametuhadithia, kutoka kwa Sulaymaan al-´Absiy, kutoka kwa ´Aliy bin Husayn: ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Mnapopita katika misikiti, basi mswalieni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni dhaifu mno. Abu Haatim na ad-Daaraqutwniy wamesema kuwa Sayf bin ´Umar at-Tamiymiy ni mwenye kuachwa. Yahyaa bin ´Abdil-Hamiyd al-Himaaniy ametuhumiwa kuziiba Hadiyth.  Abu ´Abdillaah Sulaymaan bin Abiyl-Mughiyrah al-´Absiy al-Kuufiy alikuwa mwaminifu. Aidha kunatosheleza kutokamana na Athar hii Hadiyth aliyoipokea Abu Humayd, au Abu Usayd, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Atakapokuja mmoja wenu msikitini, basi amsalimie Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na aseme:

اللهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ

”Ee Allaah! Nifungulie milango ya rehema Zako.”

Na wakati mmoja wenu atakapotoka amsalimie Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na aseme:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ

”Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kutokana na fadhilah Zako.”

Ameipokea Abu ´Awaanah (1/414) na Abu Daawuud (465).  Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan wameipokea katika ”as-Swahiyh” zao kupitia kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Zipo Hadiyth nyenginezo mfano wake ambazo zitakuja huko mbele kwenye kitabu.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 72-73
  • Imechapishwa: 06/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy