79. Athar ”Wakati mtu anapomaliza Talbiyah yake… ”

79 – Ya´quub bin Humayd bin Kaasib ametuhadithia: ´Abdullaah bin ´Abdillaah al-Umawiy ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin Swaalih bin Zaa-idah: Nimemsikia al-Qaasim bin Muhammad akisema:

”Wakati mtu anapomaliza Talbiyah yake, basi ilikuwa inapendeza kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]

[1] Dhaifu na cheni ya wapokezi wake imekatika. Ugonjwa wake ni Muhammad bin Swaalih bin Zaa-idah, ambaye ni mnyonge. ad-Daaraqutwniy (263) ameipokea Hadiyth kupitia kwake.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 72
  • Imechapishwa: 06/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy