81. Athar ”Mnapofika, basi tufuni kwenye Ka´bah mara saba… ”

81 – ´Aarim bin al-Fadhwl ametuhadithia: ´Abdullaah bin al-Mubaarak ametuhadithia: Zakariyyaa ametuhadithia, kutoka kwa Wahb bin al-Ajda´: Nimemsikia ´Umar bin al-Khattwaab akisema:

”Mnapofika, basi tufuni kwenye Ka´bah mara saba na swalini Mahali pa kusimama Rak´ah mbili. Kisha nendeni Swafaa na simameni pale mnapoweza kuiona Nyumba. Pigeni Takbiyr saba. Baina ya kila Takbiyr kuna himdi na sifa kwa Allaah, kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kujiomba du´aa mwenyewe. Fanya mfano wa hivo Marwah.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. ´Aarim, ambaye jina lake ni Muhammad bin al-Fadhwl (´Aarim ilikuwa ni jina lake la utani), ameihifadhi. Kumbukumbu yake ilibadilika muda ulivyoenda. Wapokezi wake wengine waliobaki ni waaminifu. Ibn-ul-Qayyim ameitaja katika “Jalaa’-ul-Afhaam”, uk. 263, kupitia kwa Ja´far bin ´Awn, kutoka kwa Zakariyyaa. Kwa hiyo Athar ikathibiti namna hiyo – na himdi zote njema anastahiki Allaah.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 73
  • Imechapishwa: 06/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy