8. Upotevu wa al-Halabiy ulifichuka baada ya kufa kwa al-Albaaniy

al-Halabiy hamu yake kubwa ni kuwafarikanisha Salafiyyuun katika miji mbali mbali. Anawasafisha vichwa wale wenye kutumbukia kwenye vitimbi vyake na hivyo wanaanza kuwapiga vita Salafiyyuun pale wanaposimama upande wa mpinzani wao. Mtu huyu anazugwa kwenye upotevu na uharibifu wenye kujigonga tangu alipokufa ´Allaamah al-Albaaniy na wapinzani wakubwa wa Salafiyyah wakaanza fitina. Pamoja na yote haya anawaita Salafiyyuun kuwa ni “wapetukaji mipaka”. Pengine anaashiria vilevile kuwakufurisha kwa sifa hii ambayo Allaah Amewasifu nayo mayahudi na manaswara. Wakati huo huo anashuhudia batili ya kwamba mapote manane ikiwa ni pamoja na Raafidhwah, Khawaarij na Suufiyyah walopetuka wametakasika na upetukaji. Kwa mujibu wake haijuzu kwa hali yoyote kuwasifu kuwa ni wapetukaji mipaka. Je, hivi kweli kuna yeyote katika uso wa ardhi ambaye ana upotevu wa fedheha na kujigonga kunakoangamiza mfano wa mtu huyu?

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
  • Imechapishwa: 08/01/2017