3- Kufanya Twawaaf katika Ka´bah. Ni haramu kwake na si sahihi kufanya Twawaaf ya faradhi na ya sunnah katika Ka´bah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kumwambia ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alipopata hedhi:

“Fanya yale [yote] anayofanya mwenye kuhiji isipokuwa kutufu kwenye Nyumba mpaka utwaharike.”[1]

Hata hivyo anapata kufanya mambo mengine yote ya Hajj na ´Umrah kama Sa´y baina ya Swafaa na Marwah, kusimama ´Arafah, kulala Muzdalifah na Minaa na kurusha vijiwe. Kutokana na hili mwanamke akipata hedhi baada tu ya Twawaaf au wakati wa Sa´y hakuna tatizo.

[1] Muslim (1211).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Dimaa’ at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa’ http://www.ibnothaimeen.com/all/books/article
  • Imechapishwa: 30/10/2016