78. Sharti ya pili inayomfunguza mfungaji: Kukumbuka

02 – Awe mwenye kukumbuka. Akiwa amesahau basi swawm yake ni sahihi na hahitaji kulipa kutokana na Aayah iliotangulia katika Suurah “al-Baqarah”. Vilevile kutokana na yale aliyopokea Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kusahau ambapo akala au akanywa basi aikamilishe swawm yake. Kwani hapana vyenginevyo Allaah ndiye kamlisha na kumnywesha.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim na tamko ni la Muslim.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuamrisha kuikamilisha funga yake ni dalili ya kusihi kwake. Unasibishwaji wa kulishwa na kunyweshwa kwa Allaah kunafahamisha mtu huyo kutochukuliwa hatua. Pale pale tu atapokumbuka au akakumbushwa atajizuia na atatema kile kilichomo ndani ya mdomo wake akiwa yuko na kitu kwa sababu wakati huo udhuru wake utakuwa umeondoka. Ni lazima kwa ambaye atamuona mwenye kufunga anakula au anakunywa amzindue. Amesema (Ta´ala):

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ

“Saidianeni katika wema na kumcha Allaah.”[1]

[1] 05:02

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 107-108
  • Imechapishwa: 02/03/2024