Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye alama tatu ni mnafiki.”[1]

Hapa ni kwa lengo la kukemea. Tunazipokea kama zilivyokuja na wala hatuzifasiri.

MAELEZO

Hatuzifasiri maana yake ni kwamba hatuzifasiri tafsiri za kimakosa na wala kuzipindisha maana. Kinachotakiwa ni kuzifasiri kwa tafsiri sahihi kwa mujibu wa mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwa njia ya kwamba unafiki umegawanyika unafiki wa kiitikafi na unafiki wa kimatendo.

Unafiki wa kimatendo haumtoi mwenye nayo katika Uislamu ingawa ni katika madhambi makubwa.

Unafiki wa kiitikadi unamtoa mwenye nao katika Uislamu. Endapo mnafiki huyu atatubia, basi tawbah yake inakubaliwa.

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:

”Tunazipokea kama zilivyokuja na wala hatuzifasiri.”

Haina maana kuwa hatujui maana yake, isipokuwa ni kwamba hatuyafasiri tafsiri za makosa wala hatuzipindishi manaa. Hata hivyo tunayabainisha kwa maana inayoenda sambamba na Qur-aan, Sunnah na ufahamu wa Salaf. Hivi ndivo inavyotakiwa. Wala hatuyalinganishi maandiko haya na mengine.

[1] al-Bukhaariy (33) na Muslim (59).

  • Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 169
  • Imechapishwa: 28/06/2026