7 – Kuacha kunuia kupambana jihaad katika njia ya Allaah, pale ambapo yatatimia masharti yake na kuondoka vikwazo vyake. Katika hali hiyo ima jihaad itakuwa ni lazima au inapendeza kwa baadhi ya watu ikiwa kitendo hicho hakigongani na matendo mengine ambayo ni muhimu zaidi; kwa mfano kuwatendea wema wazazi wawili. Dalili ya hilo ni maneno yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kufa na hajapigana vita na wala hajaizungumzisha nafsi yake kupigana vita, basi anakufa akiwa na chembe za unafiki.”[1]

8 – Mwenye kusikia adhaana siku ya ijumaa na akaacha kwenda mara tatu ni katika matendo ya kinafiki. ´Abdullaah bin Abiy Awfaa (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayesikia wito siku ya ijumaa na asiuendee, kisha akausikia na asiuendee, kisha akausikia na asiuendee, basi Allaah atapiga muhuri juu ya moyo wake na ataufanya moyo wake kuwa moyo wa mnafiki.”[2]

[1] Muslim (1910).

[2] al-Bayhaqiy. Ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (735).

  • Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 167-168
  • Imechapishwa: 28/06/2026