Kujikwamua na mali ya haramu

Swali: Nakuarifu kwamba mimi ni mshirika katika benki ya Marekani ambayo inafanya miamala ya ribaa. Nilipokuja kujua hilo, nilitoa baadhi ya hisa zinazohusiana nami na ndani yake kulikuwa na baadhi ya fedha zilizotokana na ribaa.

Jibu: Kushiriki katika benki za ribaa haijuzu. Kushiriki katika benki hizo haijuzu, kwa sababu zinafanya miamala ya ribaa na kushiriki humo ni katika mlango wa kushirikiana katika dhambi na uadui. Ikiwa atapata faida kutokana na hisa zake, basi inampasa atoe swadaqah faida hiyo wala asiihesabu kuwa ni mali yake. Aitoe katika njia za kheri, kama kuwasaidia baadhi ya mafakiri na masikini, kurekebisha vyoo au mambo mengine yanayowanufaisha watu. Asiifanye faida hiyo kuwa ni sehemu ya mali yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1677/كيفية-التصرف-بالاموال-الربوية
  • Imechapishwa: 28/06/2026