Swali: Kuna baadhi ya saa za ukutani katika misikiti zinazotoa sauti ya kengele ya muziki. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Inapaswa kengele hiyo iondolewe na saa ibaki kama ilivyo, lakini iondolewe hiyo kengele inayotoa sauti inayowachanganya wanaoswali na wanaosoma. Saa ibaki bila kengele, watu wataendelea kuiona, kuichunguza na kunufaika nayo katika msikiti kwa kujua nyakati. Lakini hakuna haja ya kuwepo kwa kengele kabisa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1646/حكم-الاجراس-التي-في-الساعات-الحاىطية-في-المساجد
  • Imechapishwa: 28/06/2026