Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Hili lina daraja tatu: Uislamu,

MAELEZO

Daraja maana yake ni ngazi. Kwa sababu tumesema kuwa dini ina ngazi tatu ambapo baadhi ziko juu zaidi kuliko zengine. Ngazi ya kwanza katika ngazi za dini ni Uislamu. Kisha baada yake kunafuata imani. Halafu baada yake kunafuata Ihsaan. Uislamu ni kitu kilichoenea. Imani imejibana kuliko Uislamu. Ihsaan imejibana zaidi kuliko imani. Mzunguko wa Uislamu ni mpana. Wanafiki wanaingia ndani yake wakinyenyekea juu ya Uislamu, wakaudhihirisha na wakashikamana nao kwa uinje. Wanaitwa waislamu pindi wataposwali pamoja na waislamu, wakatoa zakaah na wakafanya yale matendo ya uinje. Vilevile watatekelezewa hukumu za Uislamu duniani. Wanapata zile haki za waislamu na yanawapata yale ambayo yako dhidi ya waislamu. Lakini wao Aakhirah watakuwa kwenye tabaka la chini kabisa Motoni. Kwa sababu hawana imani. Bali walichonacho ni ule Uislamu wa nje peke yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 160
  • Imechapishwa: 04/01/2021