77. Matamshi ya Tashahhud – Tamko la ´Aaishah

6- Tashahhud ya ´Aaishah. Qaasim bin Muhammad amesema:

“´Aaishah alitufunza Tashahhud, akiashiria kwa mkono wake hali ya kusema:

التحيات، الطيبات، الصلوات، الزاكيات لله، السلام على النبي و رحمة الله و بركاته، السلام علينا و على عباد الله الصالحين، أشهد أن لا إله إلا الله و أشهد أن محمداً عبده و رسوله

“Maadhimisho, mazuri, swalah, na matendo mema yote yanamstahikia Allaah. Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu ya Mtume! Amani ishuke juu yetu na juu ya waja wema wa Allaah. Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.”[1]

[1] Ibn Abiy Shaybah (1/293), as-Sarraaj, al-Mukhallasw na al-Bayhaqiy (2/144) na tamko ni lake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 143
  • Imechapishwa: 01/01/2019