77. Hadiyth ”Allaah akusifu wewe na mume wako… ”

77 – Hajjaaj ametuhadithia: Abu ´Awaanah ametuhadithia, kutoka kwa al-Aswad bin Qays, kutoka kwa Nabiyh al-´Anziy, kutoka kwa Jaabir bin ´Abdillaah, ambaye amesema:

”Mwanamke mmoja alisema: ”Ee Mtume wa Allaah! Niswalie mimi na mume wangu.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Allaah akusifu wewe na mume wako.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Ameipokea Abu Daawuud (1533): Muhammad bin ´Iysaa ametuhadithia: Abu ´Awaanah ametuhadithia… Kupitia njia nyingine ameisimulia Sufyaan kutoka kwa al-Aswad bin Qays. Inapatikana kwa Ibn Abiy Shaybah (2/519).

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 71
  • Imechapishwa: 05/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy