78. Athar ”Muhammad alikuwa akimuombea du´aa na msamaha mtoto… ”

78 – Sulaymaan bin Harb ametuhadithia: Hammaad bin Zayd ametuhadithia, kutoka kwa Ayyuub, ambaye amesimulia:

”Muhammad alikuwa akimuombea du´aa na msamaha mtoto kama anavyomuombea du´aa mkubwa. Wakati alipoambiwa kuwa mtoto huyu hana dhambi, akasema: ”Midhali Allaah amemsamehe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) madhambi yake yaliyotangulia na yatayokuja baadaye, basi nimeamrishwa kumuombea.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Muhammad ni Ibn Siyriyn na Ayyuub ni as-Sikhtiyaaniy.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 71-72
  • Imechapishwa: 05/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy