Wale wanaowatukana wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wale wanaomtukana ´Aaishah – ambao ni Shiy´ah – hawa wanamtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anampenda yeye na anampenda baba yake. Isitoshe ´Aiaishah ana nafasi mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aliugulia nyumbani kwake, akafa kati ya kifua chake na kichwa chake kilikuwa juu ya mapaja yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – na fadhilah zake ni tukufu kwa sababu ya ukaribu wake kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kuteremka kwa Wahy kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yeye akiwa juu ya godoro lake – hakika anazo fadhilah tukufu.

Shiy´ah wanaomtukana ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) hapana shaka kwamba kwa kitendo hicho wanamfanyia uadui Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanamuudhi. Mwenye kumuudhi ´Aaishah amemuudhi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah ameteremsha utakaso wake kutokamana na yale ambayo wanafiki walimtuhumu kwayo katika tukio la uzushi:

أُولَـٰئِكَ مُبَرَّءُونَ مِمَّا يَقُولُونَ

“Hao wametakaswa na tuhuma za wanayoyasema.”[1]

Amesema (Jalla wa ´Alaa):

الْخَبِيثَاتُ لِلْخَبِيثِينَ وَالْخَبِيثُونَ لِلْخَبِيثَاتِ ۖ وَالطَّيِّبَاتُ لِلطَّيِّبِينَ وَالطَّيِّبُونَ لِلطَّيِّبَاتِ

“Maneno maovu ni kwa ajili ya watu waovu na watu waovu kwa maneno maovu, na maneno mema ni kwa ajili ya watu wema, na watu wema kwa maneno maovu.”[2]

Allaah hakuwa wa kumchagulia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwanamke msaliti juu ya godoro lake. Wakimtukana yeye basi wamemtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakimtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kumtukana Allaah (Jalla wa ´Alaa), jambo ambalo ni kufuru kubwa.

Wale wasiomtakasa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) juu ya yale waliyomtuhumu kwayo wanafiki watu hao ni makafiri. Kwa sababu ni wenye kumkadhibisha Allaah, Mtume Wake na maafikiano ya waislamu. Kabla yake Maryam bint ´Imraan alituhumiwa na mayahudi – Allaah awalaani – ambapo Allaah akamtakasa kutokamana na waliyoyasema. Shiy´ah wanafanana na mayahudi kwa njia nyingi ikiwa hii ni njia moja wapo ambayo ni mbaya zaidi.

[1] 24:26

[2] 24:26

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 110-111
  • Imechapishwa: 20/05/2021