Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema
ولا تُنكِرَنْ جهلاً نكيراً ومُنكراً
29 – Usimpinge kwa ujinga Nakiyr na Munkar
ولا الحوْضَ والِميزانَ إنك تُنصحُ
wala [usipinge] Hodhi na Mizani – hakika wewe unanasihiwa
3 – Mizani. Ni mizani ya kihakika yenye masahani mawili. Mema yatawekwa kwenye sahani moja na maovu kwenye sahani jengine. Allaah (Ta´ala) amesema:
فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ
“Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, basi hao ndio wenye kufaulu, na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, basi hao ni wale ambao wamekhasirika nafsi zao [watakuwa] kwenye [Moto wa] Jahannam ni wenye kudumu.” (23:102-103)
فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ
“Basi yule itakayekuwa mizani yake nzito, basi huyo atakuwa katika maisha ya kuridhisha, na yule itakayekuwa mizani yake khafifu, basi makazi yake [itakuwa] ni Haawiyah.” (101:06-09)
Mizani hapa bi maana matendo yake. Mame yake yatawekwa kwenye sahani moja na maovu yake yatawekwa kwenye sahani jengine. Atalipwa kutegemea na ule upande utaokuwa na uzito zaidi. Haya ni kutokana na uadilifu wa Allaah. Hamdhulumu yeyote. Bali anamlipa mtu kwa matendo yake. Ni mizani ya kihakika.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 166-167
- Imechapishwa: 13/01/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)