Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

4 – Kusema:

رَبَّنَا وَ لَكَ الْحَمْدُ

”Ee Mola Wetu! Ni Zako himdi zote.”

Itasemwa na wote.

Hili ni jambo la wajibu la nne miongoni mwa yale mambo ya wajibu ya swalah. Makusudio ya wote ni imamu, maamuma na anayeswali peke yake. Wote wanatakiwa kusema:

رَبَّنَا وَ لَكَ الْحَمْدُ

”Ee Mola Wetu! Ni Zako himdi zote.”

Kumepokelewa juu yake Sunan nne:

A – Sunnah ya kwanza:

رَبَّنَا وَ لَكَ الْحَمْدُ

”Ee Mola Wetu! Ni Zako himdi zote.”[1]

B – Sunna ya pili:

رَبَّنَاَ لَكَ الْحَمْدُ

”Ee Mola Wetu! Ni Zako himdi zote.”[2]

C – Sunna ya tatu:

اللهم ربنا ولك الحمد

”Ee Allaah! Ni Zako himdi zote.”[3]

D – Sunna ya nne:

اللهم ربنا لك الحمد

”Ee Allaah! Ni Zako himdi zote.”[4]

5 – Kusema:

سبحان ربي الأعلى

“Ametakasika Mola wangu Aliye juu kabisa.”

katika Sujuud.

Hili ni jambo la wajibu la tano miongoni mwa yale mambo ya wajibu ya swalah. Kilicho cha wajibu ni kusema hivo mara moja, kamilifu zaidi ni mara tatu, akizidisha mara saba au kumi ni bora. Akiacha kusema hivo mwa kukusudia swalah inabatilika. Akiacha kwa kusahau basi ataiunga kwa Sujuud ya kusahau.

 6 – Kusema:

رَبِّ اغْفِرْ لِي

“Mola! Nisamehe!”

baina ya Sajdah mbili.

Hili ni jambo la wajibu la sita miongoni mwa yale mambo ya wajibu ya swalah. Atasema hivo mara moja. Akikariri mara tatu ndio bora. Akiiacha na asiseme hivo kwa makusudi swalah inabatilika. Akiacha kwa kusahau atasujudu Sujuud ya kusahau.

7 – Tashahhud  ya kwanza.

Hili ni jambo la wajibu la saba miongoni mwa yale mambo ya wajibu ya swalah. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa ´Abdullaah bin Buhaynah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:

”Hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisimama baada ya kuswali Rak´ah mbili za Dhuhr na hakuketi Tashahhud kati yazo. Wakati alipomaliza swalah yake akasujudu Sujuud mbili kisha akaleta Tasliym baada ya hapo.”

Alipounga Tashahhud ya kwanza kwa kusujudu sijdah ya kusahau ikafahamisha ya kwamba sio nguzo. Kwa sababu nguzo haidondoki; ni mamoja mtu amefanya hivo kwa kusahau au kwa kukusudia. Kwa hiyo Tashahhud ya kwanza ni wajibu.

8 – Kukaa katika Tashahhud hiyo.

Hili ni jambo la wajibu la nane miongoni mwa yale mambo ya wajibu ya swalah. Kukaa katika hiyo Tashahhud ya kwanza.

[1] al-Bukhaariy (789) na Muslim (392).

[2] al-Bukhaariy (789).

[3] al-Bukhaariy (795).

[4] al-Bukhaariy (3228) na Muslim (409).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 106-108
  • Imechapishwa: 04/07/2022