Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Wanazikubali zile fadhilah na nafasi zao zilizotjwa ndani ya Qur-aan, Sunnah na maafikiano.

Wanawafadhilisha waliojitolea na kupigana vita kabla ya Ushindi – nayo ni suluhu ya Hudaybiyah – wao wana daraja kubwa zaidi kuliko wale ambao waliojitolea baadae na wakapigana. Wanawatanguliza mbele Wahajiri juu ya Wanusuraji.

Wanaamini ya kwamba Allaah aliwaambia wale waliopigana vita vya Badr – ambao walikuwa miatatu na kumi na kitu:

“Fanyeni mtakacho, kwani Nimeshawasameheni.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema kuwa:

“Hakuna yeyote kati yenu aliyekula kiapo cha utiifu chini ya mti atakayeingia Motoni.”[2]

Bali Yuko radhi nao, nao wako radhi Naye na walikuwa zaidi ya 1400.

MAELEZO

Hii ni moja katika sifa ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ni wenye ndimi zilizo salama kwa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wao ndio viumbe bora baada ya Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Hakupatapo kuwepo na wala hakutokuwepo mfano wao. Lililo la wajibu ni kuwapenda kwa ajili ya Allaah, kuwaombea radhi, kunyamazia mizozo iliyopitika kati yao na kuamini kuwa wao ndio kizazi bora kabisa.

Ni lazima kuamini ya kwamba mbora katika makhaliyfah waongofu ni Abu Bakr, kisha ´Umar, kisha ´Uthmaan halafu ´Aliy. Licha ya kwamba kuna baadhi ya watu waliovutana kidogo kama inatakiwa kumtanguliza ´Uthmaan juu ya ´Aliy au kinyume chake. Lakini hatimaye Ahl-us-Sunnah walifikia kuona kuwa kuwa ´Uthmaan ndiye watatu na kwamba ´Aliy ndiye wanne. Hili linahusiana na uongozi na ubora. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanatakiwa kuamini hivi na wajitenge mbali na mwenendo wa Raafidhwah ambao kazi yao wao ni kuwatukana Maswahabah na kuwafanyia maudhi. Vilevile wanatakiwa kujitenga mbali na mwenendo wa Nawaaswib ambao wanawaudhi watu wa nyumba ya kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa maneno na vitendo. Ahl-us-Sunnah wanatakiwa kujiepusha mbali na tabia hizi chafu.

[1] al-Bukhaariy (3007) na Muslim (2494).

[2] Muslim (2496).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 111-112
  • Imechapishwa: 03/11/2024