75. Dhikr kwa pamoja baada ya swalah tano ni Bid´ah

Swali 75: Ni ipi hukumu ya Dhikr za pamoja baada ya swalah kwa mtindo mmoja kama wanavofanya baadhi ya watu? Je, imependekezwa kusoma Dhikr kwa sauti ya juu au kusoma kimyakimya?

Jibu: Sunnah ni kusoma Dhikr kimyakimya baada ya zile swalah tano na baada ya swalah ya ijumaa baada ya Tasliym. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea katika “as-Swahiyh” zao kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba kufanya Dhikr kwa kunyanyua sauti pindi wanapoondoka watu kutoka katika swalah za faradhi ni jambo lililokuwa likifanywa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ibn ´Abbaas amesema:

“Nilikuwa nikijua kuwa watu wameondoka pindi ninaposikia hivo.”

Kuhusu kuzileta kwa pamoja kwa njia ya kwamba kila mmoja anachunga kwenda sambamba na mwenzie kuanzia mwanzo mpaka mwisho wake na akamwigiliza katika hilo, ni kitu kisichokuwa na msingi. Bali ni katika Bid´ah. Kilichowekwa katika Shari´ah wote wamtaje Allaah bila kulenga sauti kwenda sambamba mwanzo na mwisho.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 80-81
  • Imechapishwa: 20/09/2022