74. Maswahabah walimpiga vita mwenye kumnyanyua kiumbe katika daraja ya Mtume

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mtu anaweza kusema pia: Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) waliwapiga vita Banuu Haniyfah, ilihali walisilimu pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wao wanashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, walikuwa wakiadhini na kuswali.

MAELEZO

Hili ni jibu la tatu. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walipigana vita na Musaylamah na wafuasi zake. Wakahalalisha kumwagwa damu na mali zao, ilihali walikuwa wanashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni mja na ni Mtume Wake. Walikuwa wakiadhini na kuswali. Hata hivyo walimnyanyua mtu katika daraja ya unabii. Mtu asemeje kwa mwenye kumnyanyua mtu fulani katika daraja ya al-Jabbaar wa mbingu na ardhi? Je, huyu si ana haki zaidi ya kupachikwa ukafiri kuliko yule mwenye kumnyanyua kiumbe katika katika daraja ya kiumbe mwenzie? Hili ni jambo liko wazi. Lakini ni kama alivyosema Allaah (Ta´ala):

كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ

“Hivyo ndivyo Allaah anavyopiga chapa juu ya nyoyo za wale wasiojua.” (30:59)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 75
  • Imechapishwa: 25/11/2023