06 – Kutapika kwa makusudi. Ni kule kutoa kile chakula au kinywaji kilichomo tumboni kupitia njia ya mdomo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Ambaye yatamshinda matapishi basi halazimiki kulipa. Na ambaye atajitapisha basi ni lazima kwake kulipa.”

Wameipokea watano isipokuwa an-Nasaa´iy. Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Haakim.

Anafungua akikusudia kutapika ima kwa kitendo, kama vile kufinya tumboni lake au kukonyeza koo yake, au kwa kunusa, kwa mfano akanusa kitu ili aweze kutapika, au kwa kuangalia, kwa mfano akakusudia kukiangalia kitu ili kiweze kumtapisha. Hali zote hizo zinamfunguza.

Hata hivyo hakumdhuru kitu akitapika bila yeye kusababisha. Si lazima kuzuia kutapika pale anapohisi chakula kinarudi kwa sababu kufanya hivo kunaweza kumdhuru. Anachotakiwa ni yeye kuyaacha yatoke. Asijaribu kutapika wala asiyazuie yanapotaka kutoka yenyewe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 101-102
  • Imechapishwa: 27/02/2024