Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya nadhiri ni Kauli Yake (Ta´ala):

يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا

“Wale ambao wanatimiza nadhiri zao na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea.”[1]

MAELEZO

Nadhiri ni kule mtu kuilazimisha nafsi yake mwenyewe kwa kitu ambacho hakikumlazimu kwa mujibu wa msingi wa Shari´ah. Kwa mfano mtu akaweka nadhiri ya kutoa swadaqah kitu fulani. Hivyo itamlazimu kutimiza nadhiri yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuweka nadhiri ya kumtii Allaah basi amtii.”[2]

Nadhiri ni aina moja wapo ya ´ibaadah isiyofaa isipokuwa kwa Allaah pekee. Mwenye kuliwekea nadhiri kaburi, sanamu au kitu kingine basi amemshirikisha Allaah. Ni nadhiri ya maasi na shirki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuweka nadhiri ya kumuasi Allaah basi asimuasi.”[3]

[1] 76:07

[2] al-Bukhaariy (6696 na 6700).

[3] al-Bukhaariy (6696 na 6700).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 154-155
  • Imechapishwa: 31/12/2020