Ummah huu ndio wa kwanza utakaofanyiwa hesabu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Sisi ni wa mwisho na wa mwanzo wenye kutangulia siku ya Qiyaamah wataohukumiwa kabla ya viumbe wengine.”[1]

Kuna maafikiano juu yake.

Ibn Maajah amepokea kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Sisi ni Ummah wa mwisho na ni mwanzo wataofanyiwa hesabu… “[2]

Kitu cha kwanza atachofanyiwa nacho hesabu mja miongoni mwa haki za Allaah ni swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kitu cha kwanza atachofanyiwa nacho hesabu mja siku ya Qiyaamah ni swalah. Ikitengemaa, basi yatatengemaa matendo yake mengine, na ikiharibika, basi yataharibika matendo yake mengine.”

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw” na cheni ya wapokezi wake haina neno –Allaah akitaka. Yamesemwa na al-Mundhiriy katika “at-Targhiyb wat-Tarhiyb[3]” (01/246).

Kitu cha kwanza kitachohukumiwa kati ya watu ni umwagikaji wa damu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kitu cha kwanza kitachohukumiwa kati ya watu ni umwagikaji wa damu.”[4]

Kuna maafikiano juu yake.

[1] Muslim (856, 22) na tamko lake liko kwa al-Bukhaariy (876).

[2] Ibn Maajah (4290), Ahmad (01/282), (02/274, 342), al-Bayhaqiy katika “Dalaa-il-un-Nubuwwah” (05/482). al-Buuswiyriy amesema katika ”az-Zawaaid” (03/317):

”Cheni ya wapokezi hii ni Swahiyh na wanamme wake ni waaminifu.”

Ameisahihisha Shaykh al-Albaaniy.

[3] at-Tirmidhiy (413, an-Nasaa´iy (01/232) na Ibn Maajah (1426). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (01/185).

[4] al-Bukhaariy (6864) na Muslim (1678, 28).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 119
  • Imechapishwa: 29/11/2022