Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Mzani utaopima matendo una vitanga viwili na ulimi:

فَمَنْ ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ , وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُوْلَئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ

”Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, hao ndio wenye kufaulu. Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, basi hao ni wale ambao wamekhasirika nafsi zao, watakuwa katika [Moto wa] Jahannam wenye kudumishwa.”[1]

MAELEZO

Mizani ni wingi wa mzani. Mizani maana yake katika lugha ni kitu cha kupimia vitu kama ni vyepesi au vizito. Mizani maana yake katika Shari´ah ni kitu kitachowekwa na Allaah siku ya Qiyaamah kwa ajili ya kupima matendo ya waja. Ni jambo limefahamishwa na Qur-aan, Sunnah na maafikiano ya Salaf. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَمَنْ ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ , وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُوْلَئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ

”Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, hao ndio wenye kufaulu. Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, basi hao ni wale ambao wamekhasirika nafsi zao, watakuwa katika [Moto wa] Jahannam wenye kudumishwa.”

وَنَضَعُ الْمَوَازِينَ الْقِسْطَ لِيَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا ۖ وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا ۗ وَكَفَىٰ بِنَا حَاسِبِينَ

“Tutaweka mizani ya uadilifu siku ya Qiyaamah – hivyo nafsi haitodhulumiwa kitu chochote japo ikiwa uzito wa mbegu ya hardali Tutaileta. Inatosheleza Kwetu kuwa wenye kuhesabu.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Maneno mawili yanapendeza zaidi mbele ya Mwingi wa rehema, mepesi mdomoni na mazito kwenye mizani:

سبحان الله وبحمده، سبحان الله العظيم

“Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu na himdi zote ni Zake, Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu, Mtukufu.”[3]

Kuna maafikiano juu yake.

Salaf wameafikiana juu ya kuthibiti jambo hilo.

Ni mizani ya kweli ambayo ina masahani mawili. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw ambaye amesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu yule bwana mwenye kadi:

“Madaftari yatawekwa kwenye kitanga kimoja na ile kadi iwekwe kwenye kitanga kingine.“[4]

Hadiyth ameipokea at-Tirmidhiy na Ibn Maajah. al-Albaaniy amesema:

“Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.”

[1] 23:102-103

[2] 21:47

[3] al-Bukhaariy (7563) na Muslim (2694, 31).

[4] Ameipokea Ahmad (02/213), at-Tirmidhiy (2639) na Ibn Maajah (4300). Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Hibbaan (2524), al-Haakim (01/06, 529) na adh-Dhahabiy ameafikiana naye. Ni nzuri kwa mujibu wa at-Tirmidhiy. Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (135) na akasema:

”Zipo Hadiyth nyingi juu ya hilo ikiwa sio Mutawaatir.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 119-120
  • Imechapishwa: 29/11/2022