72. Kichenguzi cha nne cha swawm: Vyenye maana ya kula na kunywa

04 – Vitu vyenye maana ya kula na kunywa. Navyo ni aina mbili:

1 – Mfungaji kuvuja damu. Kwa mfano akatokwa na damu puani ambapo akavuja damu na kukamfunguza. Kwa sababu damu ndio lengo la kurutubisha chakula na kinywaji, jambo ambalo limepatikana kwa kutokwa na muda[1].

2 – Sindano za lishe ambazo zinamtosheleza mtu kutohitajia kula na kunywa. Akizitumia basi vinamfunguza. Kwa sababu, licha ya kuwa sio kula na kunywa kikweli, kunaleta maana hiyo na hivyo ikathibiti hukumu ya viwili hivyo.

Sindano za kawaida zisizo za lishe hazifunguzi. Ni mamoja mfungaji amedungwa nazo kupitia njia ya misuli au kupitia njia ya mishipa. Haijalishi kitu kama mfungaji atahisi ladha yake kooni mwake hazimfunguzi. Kwa sababu sio kula wala kunywa wala hakuleti maana ya viwili hivyo. Kwa hivyo hakuthibiti hukumu ya viwili hivyo. Kule mfungaji kuhisi ladha kwenye koo hakuzingatiwi katika siviyokuwa kula na kunywa. Kwa ajili hiyo wanazuoni wetu wamesema:

“Akikanyaga tikiti maji kwa kiganja cha nyayo za miguu yake ambapo akahisi ladha yake kooni hakutomfunguza.”

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema katika kitabu “Haqiyqat-us-Swiyaam”:

“Hakuna chochote katika dini kinachoonyesha kuwa kifunguzi – ambacho Allaah na Mtume Wake wamekifanya kuwa ni kifunguzi – ni kile ambacho kinafika katika ubongo, mwili, kilichoingia kwa ndani au kimefika tumboni na vyenginevyo vyenye maana kama hiyo ambavyo watu wenye maoni haya mbalimbali wamevifanya ndio msingi wa hukumu ya Allaah na Mtume Wake… Ikiwa hakuna dalili inayoegemeza hukumu hizi kwa Allaah na Mtume wake juu ya sifa hizi, basi ni kama kwamba mtu anasema kuwa Allaah na Mtume wake ndio ambao wamefanya kitu hichi kuwa chenye kufunguza, jambo ambalo ni kusema bila ya elimu.”

[1] Hivo ndivo nilivyokuwa naona hapo awali. Baadaye ikanidhihirikia kuwa kuchota damu hakufunguzi. Kwa sababu sio kula wala kunywa wala hakuna maana ya kula na kunywa. Msingi ni kubaki kusihi kwa swawm mpaka kubainike kuharibika kwake. Isitoshe miongoni mwa kanuni zilizothibitishwa ni kuwa yakini haiondoki kwa shaka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 100-101
  • Imechapishwa: 24/02/2024