72. Dalili kwamba kumtaka uokozi Allaah ni ´ibaadah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya kutaka kuokolewa ni Kauli Yake (Ta´ala):

إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ

“Pale mlipomuomba uokozi Mola wenu Naye akakujibuni.”[1]

MAELEZO

 Kutaka uokozi ni aina moja wapo ya ´ibaadah. Ni kule kuomba uokozi. Ni jambo linalokuwa wakati wa shida. Pindi mtu anapoingia katika shida basi anaomba uokozi kutoka kwa Allaah ili amsalimishe kutokamana na shida hiyo. Kuna aina mbili ya uokozi:

1- Kuwaomba uokozi viumbe katika mambo ambayo hakuna ayawezaye isipokuwa Allaah (´Azza wa Jall). Aina hii ni shirki. Yule mwenye kutaka uokozi kutoka kwa asiyekuwa Allaah katika majini, watu, viumbe visivyoonekana au wafu ni shirki. Kuwataka uokozi wafu, viumbe visivyoonekana katika mashaytwaan na majini ni shirki.

2- Kuwaomba uokozi viumbe walioko mbele yako, waliohai na katika mambo wanayoyaweza ni jambo linalofaa. Amesema (Ta´ala) kuhusu kisa cha Muusa:

فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ

“Akamsaidia yule ambaye katika kundi lake dhidi ya yule ambaye ni katika adui wake.”[2]

[1] 08:09

[2] 28:15

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 152
  • Imechapishwa: 31/12/2020