71. Swalah zinazoachwa na zisizoachwa safarini

Swali 71: Wametofautiana juu ya ubora wa kuswali Sunnah ya Rawaatib wakati wa kufupisha safarini. Wako waliosema kuwa inapendeza kufanya hivo. Wengine wamesema kuwa haipendezi ikiwa swalah ya faradhi imefupishwa. Unaonaje katika jambo hilo na kadhalika swalah nyenginezo zilizopendekezwa kama mfano wa swalah ya usiku?

Jibu: Sunnah kwa msafiri ni kuacha Raatibah ya Dhuhr, Maghrib na ´Ishaa pamoja na kuleta Sunnah ya Fajr. Hivo ni kwa ajili ya kumwigiliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vivyo hivyo imesuniwa kwake kuswali Tahajjud usiku na Witr safarini. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya hivo. Inahusiana pia na swalah nyenginezo zilizoachiwa ambazo zinaswaliwa kutokana na sababu kukiwemo Sunnah ya Dhuhaa, Sunnah ya wudhuu´ na swalah ya kupatwa kwa jua. Vivyo hivyo imesuniwa kwake kusujudu Sujuud ya kisomo na swalah ya mamkuzi ya msikiti akiingia msikitini kwa ajili ya kuswali au kwa ajili ya lengo jingine basi anatakiwa kuswali swalah ya mamkuzi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 74
  • Imechapishwa: 19/09/2022