70. Unaposwali Maghrib nyuma ya imamu anayeswali ´Ishaa

Swali 70: Wakati mwingine kipindi cha kukusanya kati ya Maghrib na ´Ishaa kwa sababu ya mvua inatokea wakafika kikosi cha watu na huku imamu anaswali ´Ishaa ambapo wakajiunga na imamu hali ya kudhani kuwa anaswali Maghrib. Ni kipi kinachowalazimu?

Jibu: Ni lazima kwao kukaa chini baada ya Rak´ah ya tatu na wasome Tashahhud na du´aa kisha watoe Tasliym pamoja naye. Baada ya hapo ndipo waswali ´Ishaa ili wapate fadhilah za mkusanyiko na kutekeleza kupangilia swalah, jambo ambalo ni lazima. Ikiwa imamu amekwishaswali Rak´ah moja basi wataswali pamoja naye Rak´ah zilizosalia kwa nia ya Maghrib na itasihi. Ikiwa imamu amekwishaswali Rak´ah zaidi basi wataswali naye zile Rak´ah walizowahi kisha watalipa zile Rak´ah zitazokuwa zimebaki. Vivyo hivyo endapo watajuwa kuwa anaswali ´Ishaa basi watajiunga pamoja naye kwa nia ya Maghrib na watafanyia kazi yale tuliyotaja halafu wataswali ´Ishaa baada ya hapo kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 73-74
  • Imechapishwa: 19/09/2022