71. Kuamini sehemu ya Shari´ah na kuyapinga mengine ni sawa na kuyakanusha yote

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Na mwenye kukubali yote haya na akakadhibisha kufufuliwa, anakufuru kwa maafikiano na ni halali kumwagwa damu yake na mali yake. Kama alivyosema (Ta´ala):

إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيُرِيدُونَ أَن يُفَرِّقُوا بَيْنَ اللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيَقُولُونَ نُؤْمِنُ بِبَعْضٍ وَنَكْفُرُ بِبَعْضٍ وَيُرِيدُونَ أَن يَتَّخِذُوا بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا أُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ حَقًّا ۚ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا

“Hakika wale waliomkanusha Allaah na Mtume Wake na wanataka kufarikisha kati ya Allaah na Mtume Wake na wanasema: “Tunaamini baadhi na tunawakanusha baadhi”; na wanataka kuchukua njia iliyo baina ya hayo – hao ndio makafiri wa kweli; na Tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.”” (04:150-151)

MAELEZO

Bi maana mwenye kushuhudia ya kuwa hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Mtume wa Allaah, swalah, zakaah, swawm na hajj ni wajibu. Endapo atakadhibisha kufufuliwa, ni kafiri. Allaah (Ta´ala) amesema:

زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن لَّن يُبْعَثُوا ۚ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ ۚ وَذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

“Waliokufuru wamedai kwamba hawatofufuliwa kamwe. Sema: “Bali hapana! Naapa kwa Mola wangu, bila shaka mtafufuliwa, kisha mtajulishwa kwa yale yote mliyoyatenda – na hayo kwa Allaah ni mepesi.” (64:07)

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema kuwa kuna maafikiano juu ya hilo.

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِوَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا

“Hakika wale waliomkanusha Allaah na Mtume Wake… “

Tumetangulia kuzungumzia Aayah hii. Mtunzi ameitaja kama dalili ya kwamba mwenye kuamini baadhi na akakanusha baadhi nyingine, huyo ameyakadhibisha yote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 82-83
  • Imechapishwa: 25/11/2023