71. ´Iysaa atateremka kama mmoja wa wafuasi wa Muhammad

Kuhusu kuteremka kwa ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – kama kulivyopokelewa mapokezi mengi juu ya hilo – ni jambo la haki. Lakini anateremka akiwa ni mwenye kumfuata Mtume huyu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Atahukumu kwa Shari´ah ya Uislamu, atakuwa ni mwenye kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), atamuua ad-Dajjaal, atavunja msalaba, ataweka kodi na hakutobaki isipokuwa dini ya Uislamu. Baada ya kuteremka kwa al-Masiyh hakutobaki isipokuwa Uislamu ambao umekuja na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni mwenye kuhuisha dini ya Uislamu na mwenye kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hiyo hakuna Nabii baada ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Maneno yake:

“… na Manabii.”

Kwa sababu baadhi ya makafiri wanasema kuwa Mtume anasema kuwa hakuna Nabii mwingine baada yake na hivyo hakuna kizuizi kutumilizwa Mtume kwa sababu amesema kwamba hakuna Nabii mwingine baada yake. Wanaona kuwa kilichokanushwa ni unabii na si utume. Ametakasika Allaah kutokamana na mapungufu! Mtu hawi Mtume isipokuwa ni Nabii pia. Kila Mtume ni Nabii na si kila Nabii ni Mtume. Maneno yake:

“Imani ya mja haisihi mpaka aamini Ujumbe wake na ashuhudie unabii wake.”

Ni lazima kwa mtu ashuhudie unabii na aamini utume wake. Kwa msemo mwingine kwamba yeye ni Nabii na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Utume ni kitu kilichoenea zaidi kuliko unabii. Mwenye kukataa kushuhudia kwamba yeye ni Mtume wa Allaah ni kafiri au asitambue kuwa yeye ni mwisho wa Manabii na akajuzisha kutumilizwa baada yake Mtume ni kafiri mtu huyo na akasema kuwa ujumbe wake ni wenye kuwahusu waarabu peke yake na si watu wote, kama wanavosema baadhi ya manaswara. Wale wanaoamini ujumbe Wake lakini wanasema kuwa ni Nabii kwa waarabu peke yake ni makafiri. Kwa sababu ni lazima kuamini ueneaji wa ujumbe wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 101
  • Imechapishwa: 18/05/2021