7- Shaykh na ´Allaamah Muhammad bin ´Abdillaah as-Subayyil (Hafidhwahu Allaah) – Imaam na Khatwiyb kwenye Msikiti Mtakatifu wa Makkah


Amesema (Hafidhwahu Allaah) katika dibaji yake ya kitabu “an-Naswr al- ´Aziyz ´alaa ar-Radd al-Wajiyz”:

“Himdi zote njema ni Zake Allaah na swalah na salamu zimwendee yule ambaye hakuna Nabii mwingine baada yake, Muhammad, ahli zake na Maswahabah zake.

Wa ba´d:

“Hakika muheshimiwa Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy, Ustadhw wa Chuo Kikuu cha Kiislamu al-Madiynah al-Munawwarah, ni katika wanachuoni wanaojulikana na walinganizi mashuhuri katika jamii ya kielimu Saudi Arabia. Uwezo wake ni mwenye kujulikana katika elimu ya Sunnah na kadhalika elimu nyenginezo za Kishari´ah. Ana juhudi kubwa katika kulingania katika Dini ya Allaah juu ya mfumo wa wema waliotangulia, kutetea ´Aqiydah ya Salaf sahihi na kuwaraddi Ahl-ul-Bid´ah wal-Ahwaa´ wanaoenda kinyume nayo. Haya yanatakiwa kutajwa na kushukuriwa. Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Amdumishie neema Zake na Amzidishie Tawfiyq na uimara na swalah na salamu zimwendee Mtume wetu Muhammad, ahli zake na Maswahabah zake.”[1]

Aliulizwa pia swali lifuatalo:

“Ni ipi nasaha yako kwa wale wanaokataza kanda za wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah wanaojulikana, kama mfano wa Shaykh Muhammad Amaan al-Jaamiy (Hafidhwahu Allaah) na Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy (Hafidhwahu Allaah), na wanasema kwamba kanda za wanachuoni hawa zinaamsha fitina?”

Akajibu (Hafidhwahu Allaah) ifuatavyo:

“Najilinda kwa Allaah. Najilinda kwa Allaah. Si kweli. Hakika kanda za watu hawa ni miongoni mwa kanda bora kabisa. Watu hawa wanaita katika Sunnah na kushikamana barabara na Sunnah. Hakuna yeyote anayewasema vibaya watu hawa isipokuwa mtu anayefuata matamanio yake. Wengi katika wanaowasema vibaya watu hawa ni katika watu wa vyamavyama wanaojinasibisha na vyama na mapote. Hawa ndio wanakataza mambo haya. Ama kuhusiana na wanachuoni hawa wawili, wanajulikana kushikamana barabara na Sunnah, ´Aqiydah yao ni ya Salafiyyah na ni katika watu bora kabisa.”[2]

Kuna mwanafunzi mmoja katika ndugu zetu alimpigia simu na kumuuliza maswali. Halafu akajitambulisha yeye mwenyewe na kusema kwamba ni mmoja katika wanafunzi wa Shaykh Rabiy´. Kisha Shaykh as-Subayyil akasema kumwambia:

“Hakutolewi Fatwa na Maalik yuko al-Madiynah.”

[1] Uk. 115.

[2] Kanda ”Kashf-ul-Lithaam”.