8 – Shaykh na ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Bannaa (Hafidhwahu Allaah)

Shaykh ni katika watu waliokuwa na kipaumbele kwa Shaykh Rabiy´. Walikuwa wakisafiri pamoja kwenda Sudan akiwafanyisha mazoezi ya kutoa Khutbah na mihadhara. Hata hivyo anahesabiwa ni mmoja katika waalimu wa Shaykh Rabiy´. Kila anayemjua Shaykh al-Bannaa ataona jinsi anavyomuadhimisha Shaykh Rabiy´ kwa maadhimisho makubwa kabisa. Siku moja aliingia nyumbani kwake, Shaykh al-Bannaa akasema kumwambia:

“Kaa chini na usisimame. Hata kama mimi ni mwalimu wako, wewe ndiye Ustadhw wangu.”

Shaykh al-Bannaa ana msimamo mkubwa kwa Ahl-ul-Bid´ah ambao unaonesha Ikhlaasw na mapenzi yake ya Sunnah na watu wake pamoja na kuwa na ukali kwa wanaoenda kinyume nayo. Miongoni mwa maneno yake (Hafidhwahu Allaah) kuhusu Shaykh wetu, Shaykh Rabiy´, amesema katika dibaji yake ya kitabu “Jamaa´ah Waahidah laa Jamaa´aat”:

“Ninamjua Dr. Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy tangu wakati alipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kiislamu. Alikuwa na pupa ya kutambua Sunnah, mfumo wa wema waliotangulia, na kupita juu ya uongofu wao na kulingania katika Njia hii iliyonyooka. Likizo moja hivi ya majira ya joto nilisafiri pamoja naye na ndugu ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq, ´Umar Sulaymaan al-Ashqar na Shaykh Muhammad Amaan al-Jaamiy pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Sudan ambao walikuwa na mfumo mmoja katika Da´wah Sudan. Ambaye alikuwa na uthabiti imara katika njia hii, ilikuwa ni Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy. Tunamuomba Allaah amdumishie uthabiti wake. Anatetea Sunnah na anabainisha makosa ya baadhi ya waliotumbukia ndani yake. Baadhi ya watu hawa ni wale ambao tulikuwa tukiwadhania vyema, lakini ambao watu wengi wamedanganyika nao, kama mfano wa Shaykh ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq. Amemkosoa kwa nasaha ya kitabu “Jamaa´ah Waahidah laa Jamaa´aat wa Swiraatw Waahidah laa ´Asharaat”. Humo amebainisha haki anayoona. Allaah Amjaze kwa kheri iliokuwa nzuri, Amuongoze ndugu ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq na ndugu wengine wote katika mfumo wa Njia iliyonyooka na kutulinda sote na njia zingine zote. Nimepata khabari kwamba Shaykh Muhammad Amaan al-Jaamiy (Ghafarallaahu lah) amefariki. Allaah Amuingize katika Pepo Yake. Alikuwa ni katika watetezi wa Sunnah na akiita katika mfumo wa wema waliotangulia. Ninamuomba Allaah Amkubalie juhudi Zake na Atusamehe sisi na yeye.”[1]

Aliulizwa vilevile swali lifuatalo:

“Shaykh Rabiy´ anahesabika ni katika wanachuoni wakubwa (Kibaar-ul- ´Ulamaa´)?”

Akajibu kwa kusema:

“Ni nani leo hii na hapo kabla ambaye ana ujuzi wa uhakika wa walinganizi wengi kama yeye? Ni nani? Anajua kwa dalili na hoja. Hamzungumzii yeyote isipokuwa kwa dalili. Kwa ajili hii ndio maana ninasema kuwa Rabiy´ bin Haadiy ni Yahyaa bin Ma´iyn wa leo… Mjuzi wa kuwatambua watu leo kwa dalili na hoja ni Shaykh Rabiy´ bin Haadiy (Hafidhwahu Allaah). Ninamuomba Allaah Ahifadhi akili na kumbukumbu yake. Allaah Amjaze kheri, Ampe uthabiti na Amfanye aweze kubaki zaidi ili aweze kuwaraddi wale ambao wamevaa kivazi cha Salafiyyah na wanaipiga vita. Tunamuomba Allaah Aweze kutubainishia hali zao, Awafichukue na Atuepushe na shari zao.”

[1] Tazama dibaji ya kitabu cha Shaykh Rabiy´ ”an-Naswr al-´Aziyz”.

  • Mhusika: Shaykh Khaalid bin Dhwahwiy adh-Dhwafayriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.rabee.net/ar/sharticles.php?cat=12&id=57
  • Imechapishwa: 03/12/2019